Kuwa tayari Tunisia kukabiliana na ongezeko la machafuko Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i1246-kuwa_tayari_tunisia_kukabiliana_na_ongezeko_la_machafuko_libya
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia amesema kuwa nchi yake iko tayari kukabiliana na ongezeko la machafuko huko Libya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 14, 2016 10:38 UTC
  • Kuwa tayari Tunisia kukabiliana na ongezeko la machafuko Libya

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia amesema kuwa nchi yake iko tayari kukabiliana na ongezeko la machafuko huko Libya.

Khamis Jhinaoui Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia amesema kuwa nchi yake inaandaa mpango mkuu wa kukabiliana na matukio ya Libya khususan taathira za moja kwa moja itakazopata Tunisa iwapo nchi za Magharibi zitaanzisha mashambulizi ya anga huko Libya.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia ameongeza kuwa serikali ya nchi hiyo imechukua hatua za lazima iwapo kutajiri vita huko Libya na kwamba kamati ya kitaifa chini ya usimamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo imeundwa kuhusiana na suala hilo.

Khamis Jhinaoui amesema kuwa hali ya usalama ya nchi hiyo na eneo kwa ujumla itaathirika iwapo kutajiri vita huko Libya.

Hii ni katika hali ambayo Martin Kobler Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya pia hivi karibuni alitahadharisha kuhusu kuongezeka machafuko huko Libya na kutaka kuundwa haraka serikali ya umoja wa kitaifa nchini humo ili kurejesha nguvu ya serikali.