Nigeria yasisitiza kurejeshwa uthabiti katika maeneo ya mpaka na Cameroon
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i12466-nigeria_yasisitiza_kurejeshwa_uthabiti_katika_maeneo_ya_mpaka_na_cameroon
Rais wa Nigeria amesisitiza kurejeshwa uthabiti katika maeneo ya mpaka wa nchi hiyo na Cameroon.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 02, 2016 11:16 UTC
  • Nigeria yasisitiza kurejeshwa uthabiti katika maeneo ya mpaka na Cameroon

Rais wa Nigeria amesisitiza kurejeshwa uthabiti katika maeneo ya mpaka wa nchi hiyo na Cameroon.

Rais Muhammadu Buhari ameashiria mzozo wa mpakani kati ya Nigeria na Cameroon na kuongeza kuwa nchi yake inafanya jitihada ili kupatikana amani na uthabiti katika maeneo ya mpaka wake na Cameroon. Hii ni katika hali ambayo mashambulizi  ya kundi la Boko Haram katika nchi jirani na Nigeria yameshika kasi katika siku za hivi karibuni. Huko nyuma kundi la Boko Haram liliushambulia mji wa Jamanga karibu na mpaka wa Nigeria; mji ambao umekuwa mashuhuri kutokana na kuwa na msitu wa mvua; mashambulizi ambayo yalikabiliwa na jibu la vikosi vya jeshi la Nigeria. Wakazi wengi wa mji wa Jamanga ni Waislamu.

Mji wa Amchide ambao upo karibu na mji wa Jamanka ambao ulikumbwa na hujuma za Boko Haram 

 Kuanzia mwaka 2013, kundi la wanamgambo wa kitakfiri la Boko Haram  limeshambulia mara kadhaa eneo la kaskazini mwa Cameroon.  Mji wa Jamanka uko karibu na mji wa Amchide, ambao kabla ya hapo ulikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya Boko Haram. Duru za habari za Afrika zimearifu kuwa juhudi za kieneo barani humo kwa minajili ya kuliangamiza kundi hilo zinaendelea.