Wananchi wa Morocco waandamana na kuchoma moto bendera ya Israel
Maelfu ya wananchi wa Morocco wameandamana na katika miji mbalimbali ya nchi hiyo Rabat, mji mkuu wa nchi hiyo wakilaani jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Gaza.
Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Habari la Tasnim, katika siku ya kwanza ya sikukuu ya Eid al-Adh’ha (jana Jumamosi), raia wa Morocco walifanya maandamano ya kuwapinga Wazayuni katika miji mbalimbali ya nchi hiyo, kama vile Meknes (kaskazini), Quneitra (magharibi), Oujda (mashariki), na Agadir (kusini-magharibi), kulaani mauaji ya kimbari ya miezi 20 yaliyofanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel.
Washiriki wa maandamano hayo wakiwa wamebeba picha za Msikiti wa Al-Aqswa walipiga nara za kulaani jinai za jeshi la Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza na kutaka kutumwa misaada ya kibinadamu katika Ukanda huo.
Kadhalika washiriki wa maandamano hayo sambamba na kulaani jinai na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ghaza, wametoa mwito wa kukomeshwa mara moja uhusiano wa nchi yao na Israel.
Maandamano hayo yameshika kasi katika miaka michache iliyopita hususan tangu kuanza Vita vya Gaza na jinai kubwa zinazofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi. Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, wananchi wa Morocco mbali na kulaani jinai za Israel dhidi ya Wapalestina, mara kadhaa wametoa mwito wa kufutwa makubaliano ya kuwa na uhusiano na utawala wa Kizayuni.