Nembo ya ‘Made in Tanzania' yazinduliwa katika Maonesho ya Sabasaba 2025
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i128078
Tanzania imezindua rasmi nembo ya ‘Made in Tanzania’ kwa lengo la kutangaza bidhaa zinazotengenezwa nyumbani kimataifa na kuitangaza Tanzania kama nchi ambayo inatengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu, ubunifu na hasa zenye asili ya Kiafrika.
(last modified 2025-08-15T09:14:33+00:00 )
Jul 08, 2025 12:39 UTC
  • Nembo ya ‘Made in Tanzania' yazinduliwa katika Maonesho ya Sabasaba 2025

Tanzania imezindua rasmi nembo ya ‘Made in Tanzania’ kwa lengo la kutangaza bidhaa zinazotengenezwa nyumbani kimataifa na kuitangaza Tanzania kama nchi ambayo inatengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu, ubunifu na hasa zenye asili ya Kiafrika.

Nembo hiyo ilizinduliwa siku ya Jumatatu na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam au kama yanavyojulikana Saba Saba.

Dkt. Mwinyi alikuwa katika hafla ya ufunguzi rasmi ya maonesho hayo ya 49 katika uwanja wa maonesho wa Mwalimu Julius K. Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Akizunguma katika hafla hiyo. Dkt. Mwinyi alisema nembo hiyo itakuwa chachu ya kukuza uzalendo wa kibiashara na kuhimiza raia wa Tanzania kununua bidhaa zinazotengenezwa nchini humo.

Maonesho hayo yanafanyika kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai.

Maonesho hayo ya biashara yalianza mwaka 1962 yakiwa ni maonesho ya Kilimo yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Wizara ya Biashara na Ushirika. Maonesho hayo yalikuwa na lengo la kukuza kilimo na ushirika.

Miaka ya hivi karibuni maonesho hayo yamekuwa yakishirikisha nchi takribani 20 kutoka Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) vilevile yamejulikana kama maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam na viwanja yanakofanyika vinajulikana kama viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere.../