Afrika yataka kuchukuliwa hatua madhubuti ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi
Afrika inachangia chini ya asilimia 5 ya uzalishaji wa gesi chafuzi duniani lakini inalipa kile ambacho mtaalamu mmoja wa masuala ya hali ya hewa anakiita “gharama kubwa" ya mabadiliko ya hali ya hewa; mada ambayo imetawala katika Mkutano wa Pili wa Hali ya Hewa wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Kiber Zelalem Mhadhiri wa kilimo cha bustani aliyehudhuria Mkutano wa Pili wa Hali ya Hewa mjini Addis Ababa mji mku wa Ethiopia ameeleza kuwa bara la Afrika ndilo lililoibua ajenda ya masuala yanayohusiana na hali ya hewa kwa kuwa bara hilo ndilo mhanga mkuu wa athari za mabadiliko ya tabianchi.
Amesema, mataifa ya dunai ambayo yamepiga hatua kubwa kiuchumi na kiviwanda yanapasa kuwajibika na kubeba dhima ya maafa na uharibifu unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Mhadhiri huyo wa kilimo cha bustani ameongeza kuwa Afrika inapasa kupewa nafasi ya uongozi katika uwanja huo.
Mkutano wa Pili wa Hali ya Hewa wa Afrika uliodumu kwa siku tatu mjini Addis Ababa, Ethiopia umewaleta pamoja wakuu wa nchi, jumuiya za kikanda, mashirika ya kiraia na viongozi wa biashara.
Mahmoud Ali Youssouf Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika ametoa mkutanoni akitaka kutekeleza uadilifu katika ufadhili wa kimataifa. Amesema kuwa Kamisheni ya Umoja wa Afrika inaamini kuwa fedha za ufadhili wa masuala ya hali ya hewa zinapasa kugawia kwa uadilifu na haki.
" Ufadhili wa hali ya hewa sio hisani, ni haki ya Afrika', amesema Paulino Omoj Omay, mtaalamu wa hali ya hewa katika Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa cha Jumuiya ya IGAD.