RSF yaitaka serikali ya Burundi kumwachilia huru mwandishi wa habari
Shirika na Madaktari Wasio na Mipaka (RSF), limetaka kuachiliwa huru mwandishi wa habari raia wa Burundi anayeshikiliwa na vyombo vya usalama vya nchi hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Shirika la (RSF) imekosoa hatua ya kutiwa mbaroni mwandishi wa habari Gisa Steve Irakoze wa redio ya Buja FM kwa tuhuma za kusababisha machafuko na limeitaka serikali ya Bujumbura kumuachilia huru mwandishi huyo haraka. Irakoze alitiwa mbaroni tarehe 18 mwezi huu na maafisa upelelezi wa Burundi katika mji wa Gatumba, magharibi mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura.
Kwa mujibu wa shirika hilo, hadi sasa sababu ya mwandishi huyo wa habari kutiwa mbaroni na serikali ya nchi hiyo haijawekwa wazi, isipokuwa polisi imemtuhumu Gisa Steve Irakoze kuwa amevuruga usalama wa nchi.
Ni vyema kuashiria hapa kwamba, mwandishi huyo ana uraia wa nchi mbili wa Rwanda na Burundi. Burundi na Rwanda hazina uhusiano mzuri kufuatia mivutano ya hivi karibuni baina yao.
Kwengineko Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka limeeleza wasiwasi wake juu ya hatma ya Jean Bigirimana, mwandishi mwingine wa habari aliyetiwa mbaroni tarehe 22 Julai mwaka huu kwa tuhuma za kufanya safari nyingi nchini Rwanda.