AU: Hatua zaidi zichukuliwe kuzuia vijana kufuatia itikadi za msimamo mkali Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i14479-au_hatua_zaidi_zichukuliwe_kuzuia_vijana_kufuatia_itikadi_za_msimamo_mkali_somalia
Kikosi cha Umoja wa Afrika cha Kulinda Amani Somalia (AMISOM) kimetoa wito kwa vijana kushirikiana na polisi katika kupambana na itikadi za misimamo mikali na kuimarisha amani na utulivu nchini humo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Sep 02, 2016 10:23 UTC
  • AU: Hatua zaidi zichukuliwe kuzuia vijana kufuatia itikadi za msimamo mkali Somalia

Kikosi cha Umoja wa Afrika cha Kulinda Amani Somalia (AMISOM) kimetoa wito kwa vijana kushirikiana na polisi katika kupambana na itikadi za misimamo mikali na kuimarisha amani na utulivu nchini humo.

Akizungumza kwenye mkutano wa kuhamasisha jamii kuhusu njia za kukabiliana na siasa kali mjini Beledweyne, Inspekta wa AMISOM, John Marete amesema ugaidi ni tishio kubwa sana katika juhudi za serikali ya Somalia za kuelekea kwenye amani na utulivu, na kwamba kulinda jamii ni wajibu wa mamlaka za usalama na wananchi wa kawaida.

Mkutano huo katika mkoa wa Hiran uliohudhuriwa na wawakilishi wa wafanyabiashara, vijana, na wanawake ni sehemu ya mfululizo wa mikutano inayolenga kuongeza uelewa wa umuhimu wa kupambana na vurugu zinazotokana na siasa kali, kabla ya mchakato wa uchaguzi unaotarajiwa kuanza mwezi huu.

Muda wa kuhudumu kikosi cha AMISOM nchini Somalia umerefushwa kwa mwaka mwingine mmoja ili kukabiliana na magaidi nchini humo hasa wale wa kundi la kitakfiri la Al Shabab. Aidha askari hao wa AMISOM wamepewa jukumu la kushirikiana na maafisa wa uchaguzi katika kuandaa zoezi la uchaguzi mkuu ambao umepangwa kufanyika nchini Somalia baadaye mwezi huu wa Septemba.