SAUTI: Makaburi ya Umati yazidi kushuhudiwa Burundi
Sep 08, 2016 14:02 UTC
Miili ya watu wengi imegunduliwa katika mkoa wa Muramvya katikati mwa Burundi.
Miili ya watu wengi imegunduliwa katika mkoa wa Muramvya katikati mwa Burundi. Kufuatia tukio hilo mkuu wa mkoa huo ameagiza kufanyika uchunguzi kwa lengo la kuwatambua wahanga hao sanjari na kuwafahamu watu waliotekeleza mauaji hayo. Hayo yanajiri katika hali ambayo, afisa mkuu wa shirika moja la kutetea haki za binaadamu nchini Burundi amesema kuwa, makaburi ya umati yamekuwa yakigundulika katika maeneo kadhaa nchini humo suala ambalo linatia wasi wasi mkubwa.
Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Bujumbura Bi Hamida Issa kwa taarifa kamili………./
Tags