Jenerali wa jeshi Somalia auawa katika shambulizi lililolenga msafara wake
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i15583-jenerali_wa_jeshi_somalia_auawa_katika_shambulizi_lililolenga_msafara_wake
Polisi ya Somalia imetangaza kutokea mripuko wa bomu lililotegwa garini katika mji mkuu Mogadishu ukimlenga kamanda wa jeshi la nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 18, 2016 09:50 UTC
  • Jenerali wa jeshi Somalia auawa katika shambulizi lililolenga msafara wake

Polisi ya Somalia imetangaza kutokea mripuko wa bomu lililotegwa garini katika mji mkuu Mogadishu ukimlenga kamanda wa jeshi la nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Jenerali Mohamed Roble Jimale maarufu kwa jina la Goobaanle, ameuawa katika hujuma hiyo akiwa pamoja na walinzi wake wanne. Kamanda wa polisi mjini Mogadishu Mohamed Aden amethibitisha habari hiyo na kusema kuwa gari lililokuwa limesheheni mada za miripuko na kuegeshwa barabarani, lililipuka wakati wakati wa msafara wa kijeshi uliokuwa unamsindikiza Jenerali Mohamed Roble Jimale na kupelekea mauaji hayo. Tayari kundi la kigaidi na kitakfiri la ash-Shabab limetangaza kupitia kituo cha redio cha Andalus nchini humo kuhusika na hujuma hiyo.

ash-Shabab

Kwa mujibu wa kundi hilo la kitakfiri, mwanachama wake mmoja aliyekuwa ndani ya gari hilo, amefariki dunia. Wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la ash-Shabab wamekuwa wakitekeleza hujuma za kigaidi dhidi ya askari, maafisa wa serikali, idara za serikali na hata mahoteli kwa lengo la kuitia hasara serikali ya Mogadishu ambayo wanaituhumu kuwa ya kikafiri.