AMISOM: Lazima tutawafyeka wanachama wa kundi la kigaidi la ash-Shabab Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i15601-amisom_lazima_tutawafyeka_wanachama_wa_kundi_la_kigaidi_la_ash_shabab_somalia
Msemaji wa askari wa kusimamia amani wa Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM amesisitizia udharura wa kulitokomeza kundi la kigaidi na kitakfiri la ash-Shabab nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 18, 2016 23:44 UTC
  • AMISOM: Lazima tutawafyeka wanachama wa kundi la kigaidi la ash-Shabab Somalia

Msemaji wa askari wa kusimamia amani wa Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM amesisitizia udharura wa kulitokomeza kundi la kigaidi na kitakfiri la ash-Shabab nchini humo.

Joe Kibet aliyasema hayo Jumapili ya jana ambapo sanjari na kuthibitisha habari ya kudhibitiwa na askari mji wa El-Wak ambao uko jirani na Kenya kutoka mikononi mwa wanachama wa ash-Shabab, amesema kuwa, operesheni za jeshi zimefanikiwa kugundua kiasi kikubwa cha silaha na zana nyingi za kijeshi zilizokuwa zikitumiwa na magaidi hao.

Askari wa AMISOM wakilinda amani nchini Somalia

Amesema kuwa hadi sasa mji huo uko mikononi mwa jeshi la AMISOM. Itakumbukwa kuwa askari wa Somalia kwa kusaidiwa na askari wa AMISOM waliudhibiti mji huo wa El-Wak siku ya Jumamosi iliyopita. Wakati huo huo, Rais Hassan Sheikh Mohamoud wa Somalia amesema kuwa, usalama, amani na uthabibiti wa kisiasa nchini ni mambo yenye kupewa umuhimu mkubwa na serikali yake. Hayo yanajiri katika hali ambayo Jumapili ya jana kuliripotiwa kujiri shambulizi la kigaidi dhidi ya msafara wa mmoja wa makamanda wa jeshi la Somalia katika viunga vya mji wa Mogadishu na kusababisha hasara ya mali na roho.