Wapinzani Kongo DR watakiwa kujongea kwenye mazungumzo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i17425-wapinzani_kongo_dr_watakiwa_kujongea_kwenye_mazungumzo
Jumuiya ya Ustawi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) imewataka wapinzani wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kujiunga na mazungumzo ya kitaifa ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 15, 2016 00:28 UTC
  • Wapinzani Kongo DR watakiwa kujongea kwenye mazungumzo

Jumuiya ya Ustawi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) imewataka wapinzani wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kujiunga na mazungumzo ya kitaifa ya nchi hiyo.

Idara ya Ushirikiano wa Kisiasa, Kiulinzi na Kiusalama ya Jumuiya ya SADC imetoa taarifa ikiwataka wapinzani nchini Kongo DR kushiriki kwenye mazungumzo ya kitaifa ili kufikia mapatano.

Taarifa SADC imeashiria mafanikio yaliyopatikana katika mazungumzo ya kitaifa ya Kongo na mchakato wa kuwaandikisha wapiga kura unaofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya nchi hiyo (CENI) na kuwataka viongozi wote wa kisiasa wa Kongo kuandaa mazingira mazuri ya kufanikisha uchaguzi ulio huru, wa kiadilifu, wa wazi na wenye itibari nchini humo.

Maandamanoya wapinzani Kinshasa mwezi Septemba mwaka huu yaliyosababisha vifo vya makumi ya watu

Ujumbe wa SADC umeelekea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kutathmini hali ya kisiasa na kiusalama, zikiwemo juhudi zinazofanyika kwa shabaha ya kudumisha amani na utulivu wa kisiasa nchini humo. Mazungumzo ya kitaifa ya Kongo yalisitishwa baada ya kutokea machafuko ya umwagaji damu tarehe 19 na 20 mwezi Septemba mwaka huu kufuatia maandamano ya wapinzani  yaliyofanywa na wapinzani katika mji mkuu Kinshasa.