Mwandishi wa habari Mmarekani atiwa mbaroni nchini Burundi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i18055-mwandishi_wa_habari_mmarekani_atiwa_mbaroni_nchini_burundi
Polisi nchini Burundi wamemsaili mwandishi wa habari raia wa Marekani na mtu aliyekuwa ameandamana naye kwa tuhuma ya kuharibu nyaraka zinazohusu kesi ya jinai.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Oct 24, 2016 04:46 UTC
  • Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi
    Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi

Polisi nchini Burundi wamemsaili mwandishi wa habari raia wa Marekani na mtu aliyekuwa ameandamana naye kwa tuhuma ya kuharibu nyaraka zinazohusu kesi ya jinai.

Katika taarifa yake ya jana Jumapili, polisi ya Burundi imesema, imemetia mbaroni Bi Julia Steers na raia mmoja wa Burundi aliyekua akimsaidia aliyetambuliwa kama Gildas Yihundipundu katika wilaya ya Mutakura jijini Bujumbura.

Msemaji wa Polisi, Pierre Nkuriye amesema wawili hao walikuwa wanajaribu kuharibu ushahidi kuhusiana na jinai zilizofanywa na waasi.

Serikali ya Burundi hutumia neno waasi kuashiria waandamanaji wanaopinga utawala uliopo madarakani. Wilaya ya Mutakura ilikumbwa na maadamano mwaka jana wakati Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza nia yake ya kuwania nafwasi ya urais kwa muhula wa tatu mfululizo.

Msemaji wa polisi Burundi amesema, mwandishi wa habari huyo raia wa Marekani amekabidhiwa kwa ubalozi wa nchi hiyo mjini Bujumbura lakini mwenzake Mrundi bado anashikiliwa.

Maandamno

Burundi inashuhudia mgogoro mbaya zaidi tangu vilipomalizika vita vya ndani vilivyochochewa na ukabila mwaka 2005. Mgogoro huo uliosababishwa na Rais Pierre Nkurunziza kuwania tena urais kwa muhula wa tatu umepelekea mamia ya watu kuuawa na mamia ya maelfu kuihama nchi na kuwa wakimbizi katika nchi jirani.