Maghala matatu makubwa ya silaha yanaswa Tunisia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i19444-maghala_matatu_makubwa_ya_silaha_yanaswa_tunisia
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia imeripoti kuwa, imegundua na kuzuia maghala matatu makubwa yaliyosheheni silaha za aina mbalimbali katika eneo la mpaka wa nchi hiyo na Libya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 14, 2016 11:25 UTC
  • Maghala matatu makubwa ya silaha yanaswa Tunisia

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia imeripoti kuwa, imegundua na kuzuia maghala matatu makubwa yaliyosheheni silaha za aina mbalimbali katika eneo la mpaka wa nchi hiyo na Libya.

taarifa ya wizara imesema maghala hayo matatu ya silaha yamepatikana katika eneo la Bin Qirdan yakiwa na silaha za aina tofauti kama bunduki za Kalashinkov, roketi na mabomu ya kutegwa ardhini. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, maghala hayo matatu ya silaha yamegunduliwa na vyombo vya usalama vya nchi hiyo. Kugunduliwa maghala hayo matatu makubwa ya silaha kumewatia wasiwasi viongozi wa Tunisia kuhusu uwezekano wa kuwepo tishio la kupenya magaidi wa kundi la Daesh na kuingia nchini humo wakitokea nchi jirani ya Libya. 

Magaidi wa Daesh wakiwa katika mji wa Sirte Libya

Kundi la kigaidi la Daesh ambalo linatumia vibaya hali ya mchafukoge na ukosefu wa usalama huko Libya, mwezi Machi mwaka huu lilituma makumi ya magaidi wa kundi hilo katika eneo la Bin Qairdan na kufanya shambulio dhidi ya vituo vya polisi na jeshi la nchi hiyo. Watu 53 waliuawa katika shambulizi hilo.

Hayo yote yanajiri katika  hali ambayo Tunisia imeimarisha hali ya usalama katika maeneo ya mpaka wake na Libya ili kuwazuia magaidi wa Daesh kuingia nchini huko. Inatazamiwa kuwa magaidi hao wanaokabiliwa na mashambulizi makali ya jeshi la Libya katika mji wa Sirte yumkini wakakimbilia katika nchi jirani ya Tunisia.