Mazishi ya Waislamu waliouawa kinyama na Jeshi la Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i19678-mazishi_ya_waislamu_waliouawa_kinyama_na_jeshi_la_nigeria
Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (INM) imefanya mazishi ya Waislamu waliouawa kinyama hivi karibuni na jeshi la nchi hiyo katika mji wa kaskazini wa Kano.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 17, 2016 23:53 UTC
  • Mazishi ya Waislamu waliouawa kinyama na Jeshi la Nigeria

Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (INM) imefanya mazishi ya Waislamu waliouawa kinyama hivi karibuni na jeshi la nchi hiyo katika mji wa kaskazini wa Kano.

Taarifa zinasema siku ya Jumatano,  INM ilifanya mazishi ya waliouawa katika tukio hilo, akiwemo mtoto wa miaka miwili.

Waislamu hao waliozikwa waliozikwa walikuwa miongoni mwa 100 waliouawa shahidi Jumatatu wiki hii kwa kupigwa risasi na jeshi la nchi hiyo wakati wakiwa katika matembezi ya kumbukumbu ya Arubaini ya Mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS.

Waislamu hao wa madhehebu ya Shia waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa walipokuwa katika mjumuiko huo wa kidini nje kidogo ya mji wa Kano ulioko kaskazini mwa Nigeria. Inasemekana kuwa Jeshi la Nigeria lingali linashikilia miili ya baadhi ya waliouawa katika tukio hilo.

Inafaa kukumbusha hapa kuwa, majlisi na ziara ya siku ya Arubaini hufanyika kila mwaka tarehe 20 Safar, kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria,  baada ya kupita siku Arubaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram kwa ajili ya kukumbuka kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbala.

 Desemba mwaka jana, Jeshi la Nigeria liliwashambulia wafuasi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria IMN katika mji wa Zaria jimboni Kaduna kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi lilidai kuwa wafuasi wa IMN walikuwa na njama ya kutaka kumuua Mkuu wa Jeshi la Nigeria, madai ambayo yamekanushwa vikali na wafuasi wa harakati hiyo. Jeshi hilo katili liliizika miili ya waliouawa katika kaburi moja kwa lengo la kuficha ushahidi wa ukubwa wa jinai hiyo.

Harakati ya Kiislamu ya Nigeria hata hivyo inasisitiza kuwa zaidi ya Waislamu 1000 waliuliwa na jeshi la nchi hiyo katika hujuma hiyo.