Wanaharakati wa Ghana: Uchaguzi unapasa kufanyika katika mazingira ya amani
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i20794-wanaharakati_wa_ghana_uchaguzi_unapasa_kufanyika_katika_mazingira_ya_amani
Wanaharakati wa kisiasa nchini Ghana wamesisitiza juu ya ulazima wa kufanyika uchaguzi mkuu katika mazingira ya amani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 05, 2016 11:35 UTC
  • Wanaharakati wa Ghana: Uchaguzi unapasa kufanyika katika mazingira ya amani

Wanaharakati wa kisiasa nchini Ghana wamesisitiza juu ya ulazima wa kufanyika uchaguzi mkuu katika mazingira ya amani.

Wanaharakati hao wa kisiasa na vyama vinavoshiriki kwenye uchaguzi wa Rais na Bunge huko Ghana leo wamesaini hati ya mapatano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Accra na kusisitiza ulazima wa kufanyika uchaguzi katika hali ya amani. 

Wanaharakati hao wametilia mkazo udharura wa kuzuia kutokea aina yoyote ya machafuko kutoka kwa wafuasi wa wagombea wa makundi nbalimbali wanaoshiriki katika uchaguzi huo na wametaka kudhaminiwa kikamilifu ulinzi na usalama na kuzingatiwa madai ya ya kisheria ya wanaharakati wote wa kisiasa. Tume ya Uchaguzi ya Ghana tayari imeitisha kikao maalumu kilichohudhuriwa na wawakilishi wa vyama na mirengo mbalimbali ya kisiasa na kusisitiza kuwa, kufanyika uchaguzi wa Rais na Bunge katika mazingira ya amani na ya uwazi kunaweza kuandaa njia ya ustawi na maendeleo ya kisiasa nchini humoa.

Rais wa sasa wa Ghana, John Dramani Mahama ambaye alishika hatamu za uongozi mwaka 2013 baada ya kuaga dunia rais wa wakati huo, John Atta Mills, atachuana na kiongozi wa upinzani Nana Akufo-Addo katika uchaguzi wa Rais na Bunge uliopangwa kufanyika keshokutwa tarehe 7 Disemba. Nana Akufo-Addo alipigwa mweleka katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2012. 

John Dramani Mahama Rais wa sasa wa Ghana (Kushoto pichani) na Nana Akufo Addo kiongozi wa upinzani (Kulia)