Dec 16, 2016 15:51 UTC
  • 11 wauliwa katika kituo cha jeshi cha upekuzi nchini Burkina Faso

Wanajeshi kumi na polisi mmoja wameuawa leo kaskazini mwa Burkina Faso baada ya watu wenye silaha wasiofahamika kukishambulia kituo cha upekuzi cha jeshi.

Shambulizi hilo limetajwa kuwa la nadra kutokea huko Burkina Faso tangu kujiri shambulizi la wanamgambo wa al Qaida katika hoteli moja huko Ouagadougou mwezi Januari mwaka jana lililouwa watu 29.

Hoteli ya Splendid iliyoshambuliwa mwaka jana na watu wenye silaha mjini Ouagadougou, Burkina Faso

Shambulizi hilo la leo limefanyika kwa muda wa sasa 11 asubuhi kwa saa za Burkina Faso katika eneo lililoko umbali wa kilomita 30 kutoka katika mpaka wa Mali; na lilifanywa na watu wenye silaha wasiopungua 40 ambao hadi sasa bado hawajatambuliwa.

Itakumbukwa kuwa, kundi jipya la wanamgambo linaloongozwa na mpiganaji mmoja ambaye alikuwa mtiifu kwa raia wa Nigeria kwa jina la Mokhtar Belmokhtar lilidai kuhusika na shambulio lililofanywa mwezi Septemba katika kituo cha kijeshi huko Burkina Faso.

 

Tags