AU yataka kuhitimishwa haraka mgogoro wa Burundi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i2242-au_yataka_kuhitimishwa_haraka_mgogoro_wa_burundi
Viongozi wa Umoja wa Afrika waliozuru Burundi hivi karibuni, wametaka yafanyike mazungumzo ya haraka kati ya serikali na wapinzani, kwa lengo la kuhitimisha mgogoro wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 01, 2016 12:15 UTC
  • AU yataka kuhitimishwa haraka mgogoro wa Burundi

Viongozi wa Umoja wa Afrika waliozuru Burundi hivi karibuni, wametaka yafanyike mazungumzo ya haraka kati ya serikali na wapinzani, kwa lengo la kuhitimisha mgogoro wa nchi hiyo.

Viongozi hao wa Kiafrika wameyasema hayo kupitia ripoti waliyoitoa kufuatia ziara yao nchini Burundi ambapo wamezitaka pande husika katika mgogoro wa nchi hiyo kufanya mazungumzo ya haraka na bila ya masharti yoyote, kupitia fremu ya makubaliano ya amani ya mjini Arusha, Tanzania yaliyohitimisha vita vya ndani vya kati ya mwaka 1993-2006. Aidha ripoti hiyo imemtaka Rais Yoweri Museveni wa Uganda, ambaye kwa sasa ndiye mpatanishi wa mgogoro wa Burundi, kutangaza tarehe Mosi Machi kuwa siku ya kuanza mazungumzo baina ya pande husika. Ujumbe huo ulioongozwa na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini huku ukiwajumuisha marais wa Mauritania, Senegal, Gabon na Ethiopia, ulifanya safari nchini Burundi kati ya Alkhamis na Ijumaa iliyopita na kufanya mazungumzo na Rais Pierre Nkurunziza na wapinzani kwa lengo la kuupatia ufumbuzi mgogoro wa miezi 10 sasa nchini humo.