Rais wa Tunisia: Yamkini Israel ilimuua mhandisi wa drone za Hamas
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i22657-rais_wa_tunisia_yamkini_israel_ilimuua_mhandisi_wa_drone_za_hamas
Rais wa Tunisia amesema kuna uwezekano mkubwa kuwa utawala haramu wa Israel ulihusika katika mauaji ya mhandisi Mtunisia Mohammad Zaouari ambaye alikuwa mtegenezaji wa ndege zisizo na rubani au drone za harakati ya kupigania ukombozi wa Palestina, Hamas.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Jan 02, 2017 11:38 UTC
  • Rais Beji Caid Essebsi wa Tunisia
    Rais Beji Caid Essebsi wa Tunisia

Rais wa Tunisia amesema kuna uwezekano mkubwa kuwa utawala haramu wa Israel ulihusika katika mauaji ya mhandisi Mtunisia Mohammad Zaouari ambaye alikuwa mtegenezaji wa ndege zisizo na rubani au drone za harakati ya kupigania ukombozi wa Palestina, Hamas.

Akizungumza jana Jumapili katika hotuba ya kuanza mwaka mpya wa 2017, Rais Beji Caid Essebsi amesema "kuna uwezekano kuwa Israel ilihusika na mauaji ya mhandisi wa Hamas".

Essebsi amesema uchunguzi kuhusu mauaji hayo ungali unaendelea huku akikanusha tuhuma kuwa serikali ya Tunisia inapuuza jambo hilo.

Zaouari alipigwa risasi na kuuawa nje ya nyumba yake katika mji wa bandari ya Sfax nchini Tunisia mnamo Disemba 15 mwaka jana. Aliyehuska na mauaji hayo alitoroka na hajapatikana hadi sasa.

Mohammad Zaouari

Mtaalamu huyo wa masuala ya anga wa Tunisia alikuwa akishirikiana na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) katika kutengeneza ndege zisizo na rubani (drones)

Mauaji ya mhandisi huyo wa Tunisia yamezusha utata mkubwa na kuna uwezekano shirika la ujasusi la Israel Mossad ndilo lililopanga na kutekeleza jinai hiyo na kigaidi.

Miaka 8 iliyopita pia shirika la ujasusi la Israel, Mossad lilimuua kigaidi Khalil al Wazir maarufu kwa jina la Abu Jihad ambaye alikuwa kamanda wa harakati ya Palestina ya Fat'h akiwa nyumbani kwake katika kitongoji cha Sidi Bousaid kaskazini mwa mji mkuu wa Tunisia, Tunis.