Jeshi la Nigeria: Boko Haram wanapatiwa silaha na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i22789-jeshi_la_nigeria_boko_haram_wanapatiwa_silaha_na_israel
Duru za Nigeria zimefichua kuwa, kundi la wanamgambo wa kigaidi wa Boko Haram limekuwa likipata misaada ya silaha kutoka kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2026-01-14T11:42:18+00:00 )
Jan 04, 2017 04:28 UTC
  • Wanamgambo wa Boko Haram
    Wanamgambo wa Boko Haram

Duru za Nigeria zimefichua kuwa, kundi la wanamgambo wa kigaidi wa Boko Haram limekuwa likipata misaada ya silaha kutoka kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Jeshi la Nigeria limenukuliwa likitangaza kuwa, wanajeshi wa nchi hiyo walifanikiwa kukamata silaha nyingi katika msitu wa Sambisa uliokuwa ngome kuu ya wanamgambo wa Boko Haram na kwamba, utafiti unaonyesha kuwa, silaha hizo zimetoka moja kwa moja Israel.

Baada ya uchunguzi tumegundua kwamba, wanamgambo wa Boko Haram wamekuwa wakipata msaada wa silaha kutoka Israel, imeeleza taarifa ya jeshi la Nigeria.

Miongoni mwa silaha zilizokamatwa na jeshi la Nigeria na zinazoonesha kuwa zimetengenezwa Israel ni pamoja na bunduki, mizinga na makombora.

Wanajeshi wa Nigeria katika msitu wa Sambisa

Siku chache zilizopita Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria alitangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kuwatimua wapiganaji wa kundi la Boko Haram katika ngome yao ya mwisho huko kaskazini mashariki mwa Nigeria na kwamba magaidi hao hawatakuwa tena na maeneo ya kujificha.

Uasi na mashambulizi ya miaka 7 sasa ya kundi la kigaidi la Boko Haram yameua zaidi ya watu elfu 20 na kuwalazimisha mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi.