Jan 14, 2017 07:12 UTC
  • Rais wa Nigeria aomboleza kifo cha Ayatullah Rafsanjani

Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amemtumia salamu za rambi rambi mwenzake wa Iran kufuatia kuaga dunia Ayatullah Hashemi Rafsanjani, Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran.

Katika ujumbe wake huo, Rais Buhari amesema: "Ayatullah Hashemi Rafsanjani alikuwa mwanasiasa mkubwa mwenye taathira na ambaye alikuwa na nafasi muhimu katika maendeleo na ustawi nchini Iran."

Buhari amesema kwa kuaga dunia Hashemi Rafsanjani, Iran imepoteza mwanamapinduzi mkubwa na ulimwengu wa Kiislamu umempoteza mwanasiasa hodari. Ameongeza kuwa, kuondoka Rafsanjani kutapelekea kuibuka pengo kubwa katika uga wa kisiasa na kijamii nchini Iran.

Rais Buhari wa Nigeria

Rais wa Nigeria ameongeza kuwa: 'Mafanikio aliyoyapata Hashemi Rafsanjani yatabakia kwa muda mrefu na atakumbukwa kwa mafanikio hayo."

Ayatullah Akbar Hashemi Rafsanjani  aliaga dunia Jumapili katika hospitali moja mjini Tehran kufuatia matatizo ya moyo. Mwanasiasa na mwanazuoni huyo maarufu wa Kiislamu nchini Iran aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 82 baada ya umri mrefu wa jihadi na jitihada zisizo na kikomo kwa ajili ya Uislamu na Mapinduzi ya Kiislamu.

Tags