Wanajeshi wa UN waondoka Kodivaa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i24965-wanajeshi_wa_un_waondoka_kodivaa
Wanajeshi wa kofia bluu wa Umoja wa Mataifa wanaondoka huko Kodivaa licha ya nchi hiyo kuathiriwa na ukosefu wa amani.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 10, 2017 15:45 UTC
  • Wanajeshi wa UN waondoka Kodivaa

Wanajeshi wa kofia bluu wa Umoja wa Mataifa wanaondoka huko Kodivaa licha ya nchi hiyo kuathiriwa na ukosefu wa amani.

Wanajeshi hao wanaondoka nchini Ivory Coast kutokana na kumalizika muda uliokuwa umepangwa wa kuwepo nchini humo. 

Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast, Bi Aichatou Mindaoudou amesema kuwa kikosi cha kulinda amani cha umoja huko nchini Kodivaa kitaondoka nchini kuanzia Februari 15 mwaka huu. Aichatou ametaka kuwepo ushirikiano zaidi kati ya washirika, nchi jirani na serikali ya Ivory Coast.

Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa UN nchini Ivory Coast ameitolea mwito jamii ya kimataifa kuiunga mkono serikali ya Ivory Coast kwa kuzingatia hali ya usalama inayolegalega ya nchi hiyo kufuatia upinzani na malalamiko ya wanajeshi.

Mwezi uliopita, wanajeshi waliokuwa katika mji wa Bouake, mji mkubwa zaidi huko Kodivaa walianzisha uasi wakidai kuongezewa mishahara yao. Wanajeshi hao walisababisha hali ya taharuki katika mji huo kwa kufyatua risasi ovyo.

Uasi wa jeshi Kodivaa 

Itakumbukwa kuwa, Umoja wa Mataifa mwezi Oktoba mwaka jana ulikubaliana na serikali ya Kodivaa kuhusu kuondoka nchini humo wanajeshi wa kofia bluu na kutangaza kuwa, utaipatia nchi hiyo msaada wa kifedha wa dola milioni 50 ili kusaidia ustawi endelevu na kurejesha utawala wa sheria nchini humo.