UNICEF: Hali ya watoto barani Afrika inasikitisha
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i25510-unicef_hali_ya_watoto_barani_afrika_inasikitisha
Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetahadharisha kuhusu hali mbaya ya watoto barani Afrika.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 23, 2017 03:04 UTC
  • UNICEF: Hali ya watoto barani Afrika inasikitisha

Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetahadharisha kuhusu hali mbaya ya watoto barani Afrika.

Taarifa iliyotolewa na UNICEF imesema kuwa: Zaidi ya watoto milioni moja na laki nne watafariki dunia kutokana na njaa katika nchi za Nigeria, Somalia na Sudan Kusini katika mwaka huu wa 2017.

Taarifa hiyo imesema kuwa, watoto laki nne na nusu wanasumbuliwa na njaa kali katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria. UNICEF pia imesema kuwa, huko Somalia watoto laki moja 85 elfu wanasumbuliwa na njaa na kwamba idadi hiyo itafikia laki mbili na 70 katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo.

Hali hiyo pia imeripotiwa katika nchi ya Sudan Kusini ambako taarifa zinasema kuwa, malaki ya watoto wadogo wanasumbuliwa na utapiamlo.

Watoto wa Afrika wanasumbuliwa na utapiamlo

Imepangwa kuwa mwezi ujao wa Machi ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa utatembelea nchi za Nigeria, Cameroon, Chad na Niger kwa ajili ya kuelekeza macho ya walimwengu katika mgogoro wa kibinadamu unaowasumbua raia wa nchi hizo.