Sauti, Ripoti ya matukio ya Kiislamu yaliyojiri ndani ya siku saba zilizopita
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i27430-sauti_ripoti_ya_matukio_ya_kiislamu_yaliyojiri_ndani_ya_siku_saba_zilizopita
Ripoti ya matukio ya Kiislamu kuanzia kadhia ya malalamiko ya Mashirika na asasi za kutetea haki za binaadamu zilizotoa kilio kwa serikali ya Tanzania kutokana na kuendelea kuwashikilia korokoroni shakhsia mbalimbali wa Kiislamu nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 07, 2017 12:17 UTC

Ripoti ya matukio ya Kiislamu kuanzia kadhia ya malalamiko ya Mashirika na asasi za kutetea haki za binaadamu zilizotoa kilio kwa serikali ya Tanzania kutokana na kuendelea kuwashikilia korokoroni shakhsia mbalimbali wa Kiislamu nchini humo.

Hayo yamekuja baada ya viongozi kadhaa wa Kiislamu kutoka Zanzibar kushikiliwa kwa zaidi ya miaka mitatu sasa bila kusomewa mashitaka dhidi yao, kitendo ambacho kimetafsiriwa kuwa ni ukiukaji wa wazi wa haki za binaadamu.

Watalii ambao wamekuwa wakichafua maadili ya Kiislamu kwa kisingizio cha utalii

Kadhalika kuna kadhia ya watalii ambao bila kuzingatia heshima na utamaduni wa Kiislamu, wamekuwa wakitembea uchi katika maeneo ya Waislamu kwa madai kuwa wao ni watalii. Ni ripoti iliyoandaliwa na mwandishi wetu wa Zanzibar Hassan Issa Ali…………../