Makamu wa Rais Afrika Kusini asusia kula kuwaunga mkono Wapalestina waliogoma kula
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i29132-makamu_wa_rais_afrika_kusini_asusia_kula_kuwaunga_mkono_wapalestina_waliogoma_kula
Makamu wa rais wa Afrika Kusini na mawaziri wengine nchini humo wamesusia chakula kama njia ya kuonyesha kufungamana kwao na Wapalestina waliogoma kula katika jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
May 15, 2017 09:40 UTC
  • Makamu wa Rais Afrika Kusini asusia kula kuwaunga mkono Wapalestina waliogoma kula

Makamu wa rais wa Afrika Kusini na mawaziri wengine nchini humo wamesusia chakula kama njia ya kuonyesha kufungamana kwao na Wapalestina waliogoma kula katika jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Afrika Kuisni, SABC, Naibu wa Rais Cyril Ramaphosa, Waziri wa Mawasiliano Ayanda Dlodlo na Waziri wa Afya Aaron Motsoaledi walianza kususia chakula kwa masaa 24 kuanzia saa 12 jioni Jumapili na kumaliza Jumatatu. Viongozi hao wa Afrika Kusini wanaussia chakula kwa ajili ya kuonyesha kufungamana kwao na wafungwa 1,600 Wapalestina ambao kwa karibu mwezi mmoja sasa wamekuwa wakigoma kula chakula kama njia ya kulalamikia udhalimu wanotendewa katika jela 200 za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Taasisi ya Ahmed Kathrada, ikiungwa mkono na maveterani wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, imetoa wito kwa watu wa Afrika Kusini kujiunga na harakati yao hiyo ya kuwatetea Wapalestina wanaokandamizwa na utawala wa kibaguzi wa Israel.

Wafungwa Wapalestina

Chama tawala cha Afrika Kusini ANC kimetangaza kulaani vikali hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuwakamata kiholela wapigania ukombozi wa Palestina na kuwashikilia katika korokoro pasina kuwafungulia mashtaka na kusema mbinu hizo zinafanana na zile za utawala wa ubaguzi wa rangi katika zama za makaburu nchini humo.

Jumla ya wafungwa 1,600 wa Kipalestina wanaoshikiliwa na utawala ghasibu wa Israel, walianzisha mgomo wa kula chakula tangu tarehe 17 Aprili, katika kulalamikia miamala mibaya na kukanyagwa haki zao za kimsingi katika jela za Israel.