May 18, 2017 07:21 UTC
  • Mapigano yaendelea CAR, watano wauawa na makumi wajeruhiwa

Mapigano yameendelea kushuhudiwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ambapo watu wasiopungua watano wanaripotiwa kuuawa na makumi ya wengine wamejeruhiwa.

Ripoti zinasema kuwa, mapigano baina ya kundi la wanamgambo wa Kikristo wenye misimamo mikali wa Anti-Balaka na kundi la Seleka yameendelea kushuhudiwa nchini humo na kuzidi kuzorotesha hali ya usalama na amani katika nchi hiyo.

Mapigano na machafuko katika Jamhuri ya Afrika ya Kati yamepelekea kuongezeka wimbi la wakimbizi wanaolazimika kuyakimbia makazi yao.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, maelfu ya wakimbizi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wameelekea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, jana wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu waligundua miili 115 katika mji wa Bangassou, huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, siku chache baada ya genge la waasi wa Kikristo la Anti-Balaka kuvamia mji huo.ant

Magaidi wa Anti-Balaka

Inaelezwa kuwa, taharuki ingali imetanda katika mji wa Bagassou huku mamia ya watu wakijificha katika msikiti mmoja mjini hapo na wengine zaidi ya elfu moja wakitafuta hifadhi karibu na kituo cha UN katika mji wa Bria, yapata kilomita 300 kusini mashariki mwa Bagassou.  

Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika mgogoro, mwaka 2013 baada ya kuzuka mapigano ya kikaumu yaliyopelekea kuondolewa madarakani serikali ya rais François Bozizé. 

Tags