May 23, 2017 03:18 UTC
  • Mfumo wa usomeshaji Qur'ani katika skuli za Algeria kufanyiwa marekebisho

Katibu Mkuu wa Wizara ya Masuala ya Dini na Waqfu katika mkoa wa Ghardaia nchini Algeria ametangaza kuwa mfumo wa usomeshaji Qur'ani katika skuli za nchi hiyo utafanyiwa marekebisho kwa ushirikiano na wadau wa masuala ya kidini nchini humo.

Ridhwan Ma'ash Al-Jumuah, Katibu Mkuu wa Wizara ya Masuala ya Dini na Waqfu katika jimbo Ghardaia ameyasema hayo katika mkutano wa pili wa kitaifa wa Usomeshaji Qur'ani Tukufu ambao umefanyika kwa kaulimbiu ya "Mbinu za Usomeshaji Qur'ani; Malengo na Nyenzo".

Ma'ash Al-Jumua'h amebainisha kuwa hatua hiyo inachukuliwa kwa lengo la kuimarisha umoja wa kidini kwa ushirikiano wa wadau na wanaharakati wa masuala ya kidini.

Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Tehran ambapo washiriki kutoka Algeria walifanya vizuri

Inafaa kuashiria hapa kuwa mkutano wa pili wa kitaifa wa Usomeshaji Qur'ani Tukufu umefanyika katika jimbo la Ghardaia lililoko kusini mwa Algeria kwa kuhudhuriwa na Mashekhe, Maimamu wa Sala ya Ijumaa na Wanaakademia wa Vyuo Vikuu kwa madhumuni ya kubuni mbinu na utaratibu wa aina moja wa usomeshaji Qur'ani Tukufu.

Washiriki wa mkutano huo wamehudhuria mafunzo ya amali na kubadilishana mawazo juu ya mustakabali wa usomeshaji Qur'ani na mbinu za kujadidisha usomeshaji huo kwa kufuata misingi ya kadiri na wastani.../ 

Tags