Polisi Nigeria yatumia mabavu kuzima maandamano ya Waislamu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i29458-polisi_nigeria_yatumia_mabavu_kuzima_maandamano_ya_waislamu
Kwa mara nyingine tena polisi nchini Nigeria imetumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha kutawanya maandamano ya wananchama wa Harakati ya Kiislamu nchini humo wanaoshinikiza kuachiwa huru kiongozi wao, Sheikh Ibrahim Zakzaky.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 23, 2017 02:39 UTC
  • Polisi Nigeria yatumia mabavu kuzima maandamano ya Waislamu

Kwa mara nyingine tena polisi nchini Nigeria imetumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha kutawanya maandamano ya wananchama wa Harakati ya Kiislamu nchini humo wanaoshinikiza kuachiwa huru kiongozi wao, Sheikh Ibrahim Zakzaky.

Abdu Rahman Abubakar, mmoja wa viongozi wa harakai hiyo aliyeshiriki maandamano hayo ya jana katika mji mkuu Abuja, ameiambia kanali ya televisheni ya Press TV kuwa, hawatachoka kuandamana hadi pale vyombo vya dola vitakapotekeleza matakwa yao yanayoendana na agizo la mahakama.

Amesema licha ya muhula uliotolewa na Mahakama ya Federali Disemba mwaka jana kwa ajili ya kuachiliwa huru msomi huyo wa kidini kumalizika tarehe 16 Januari mwaka huu, lakini serikali haijatekeleza amri hiyo na inaendelea kumzuilia mwanaharakati huyo chini ya mazingira magumu bila kujali hali yake mbaya ya afya.

Waislamu wakiandamana Abuja kushinikiza kuachiwa huru Sh. Zakzaky

Kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa tarehe Pili Disemba mwaka jana na mahakama hiyo, kitendo cha kuendelea kushikiliwa na serikali ya nchi hiyo Sheikh Zakzaky, mkewe na wanaharakati wengine wa Kishia ni kinyume cha sheria.

Sheikh Zakzaky alikamatwa na jeshi la Nigeria mwezi Disemba 2015 baada ya kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na jeshi hilo, na tangu wakati huo hadi hivi sasa serikali ya nchi hiyo inayoongozwa na Rais Muhammadu Buhari inaendelea kumshikilia kinyume cha sheria, licha ya makelele kutoka ndani na nje ya nchi.