Magaidi wa Al Qaeda walilewa kabla ya kuvamia Kodivaa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i3124-magaidi_wa_al_qaeda_walilewa_kabla_ya_kuvamia_kodivaa
Magaidi wa Al Qaeda waliingia katika baa moja na kunywa pombe kabla ya kuanza kufyatua risasi kiholela katika eneo la kitalii kwenye ufukwe wa bahari nchini Ivory Coast ambapo watu wasiopungua 18 waliuawa katika mji wa Grand-Bassam.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 15, 2016 11:47 UTC
  • Magaidi wa Al Qaeda walilewa kabla ya kuvamia Kodivaa

Magaidi wa Al Qaeda waliingia katika baa moja na kunywa pombe kabla ya kuanza kufyatua risasi kiholela katika eneo la kitalii kwenye ufukwe wa bahari nchini Ivory Coast ambapo watu wasiopungua 18 waliuawa katika mji wa Grand-Bassam.

Maelezo ya hujuma hiyo yameanza kubainika ambapo walioshuhudia wanasema magaidi hao wa kund linalojiita Al al-Qaeda katika Maghreb ya Kiislamu AQIM waliwasili na gari katika baa ya ufukwe wa bahari Jumapili mchana. Wawili walibakia nje na wawili wakaingia ndani ya baa na kunywa pombe kwa muda wa nusu saa na punde baada ya hapo wakatekeleza hujuma yao ya kigaidi. Imearifiwa kuwa walianza kufyatua risasi ndani ya baa hiyo kabla ya kuelekea katika ufukwe wa bahari na kuendeleza ukatili na kuwaua watu 18 wakiwemo raia wa Burkina Faso, Cameroon, Ufaransa, Ujerumani na Mali.

Magaidi wa al Qaeda wamekuwa wakidai eti ni Waislamu lakini wasomi wa Kiislamu kote duniani wanasisitiza kuwa magaidi wa kundi hilo na wa makundi mengine kama vile ISIS au Daesh hawana mfungamano wowote na dini tukufu ya Kiislamu.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea Cote d’Ivoire, siku ya Jumapili. Ban Ki-moon ametuma salamu zake za rambi rambi kwa familia za wahanga, raia na serikali ya Cote d’Ivoire.