Wamisri 292 wafikishwa mahakamani kwa tuhuma ya kutaka kumuua al Sisi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i31570-wamisri_292_wafikishwa_mahakamani_kwa_tuhuma_ya_kutaka_kumuua_al_sisi
Watu 292 wa Misri wamefikishwa katika mahakama ya kijeshi ya nchi hiyo kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Daesh na kupanga njama ya kutaka kumuua Rais wa nchi hiyo, Abdul Fattah al Sisi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 10, 2017 01:34 UTC
  • Wamisri 292 wafikishwa mahakamani kwa tuhuma ya kutaka kumuua al Sisi

Watu 292 wa Misri wamefikishwa katika mahakama ya kijeshi ya nchi hiyo kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Daesh na kupanga njama ya kutaka kumuua Rais wa nchi hiyo, Abdul Fattah al Sisi.

Afrisa mmoja wa Misri amesema kuwa, watuhumiwa hao ambao walitangaza baia na utiifu wao kwa kundi la kigaidi la Daesh, wameunda makundi 22 ya kigaidi katika mkoa wa Sinai Kaskazini. 

Amesema kuwa, watu hao wanakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupanga njama ya kutaka kumuua Rais wa Misri. 

Wanachama wa makundi ya kigaidi, Sinai

Awali ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Misri ilikuwa imetangaza kuwa, kundi hilo lilipanga njama ya kumuua Rais Abdul Fattah al Sisi mara mbili, moja akiwa katika ibada ya Umra huko Saudi Arabia Agosti mwaka 2014 na nyingine mjini Cairo.

Kwa sasa kuna makundi kadhaa ya kigaidi katika mkoa wa Sinai Kaskazini nchini Misri mashuhuri zaidi ni lile linalojiita Wilaya ya Sinai lenye uhusiano na kundi la kigaidi la Daesh.