UN yataka kufanyika uchunguzi kuhusu mauaji ya wafungwa Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i31962-un_yataka_kufanyika_uchunguzi_kuhusu_mauaji_ya_wafungwa_libya
Umoja wa Mataifa umelitaka Jeshi la Taifa la Libya linalodhibiti eneo la mashariki mwa nchi hiyo kufanya uchunguzi kuhusu mauaji ya papo na hapo ya wafungwa.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 19, 2017 06:29 UTC
  • UN yataka kufanyika uchunguzi kuhusu mauaji ya wafungwa Libya

Umoja wa Mataifa umelitaka Jeshi la Taifa la Libya linalodhibiti eneo la mashariki mwa nchi hiyo kufanya uchunguzi kuhusu mauaji ya papo na hapo ya wafungwa.

Msemaji wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Liz Throssell amesema kuwa, kuna wasiwasi kwamba watu waliowekwa jela baada ya mapigano ya hivi karibuni katika mji wa Benghazi wanakabiliwa na hatari kuteswa na kuuawa.

Liz Throssell amesema kuwa, mwezi Machi mwaka 2017 Jeshi la Taifa la Libya lilitangaza kuwa litafanya uchunguzi kuhusu jinai za kivita ambazo huwenda zilifanywa nchini humo lakini hadi sasa hakuna habari yoyote kuhusu suala hilo.

Mapigano ya ndani Libya

Mji wa Benghazi umekuwa uwanja wa mapigano makali baina ya Jeshi la Taifa la Libya na wapiganaji wa Baraza la Mapinduzi la Benghazi lenye uhusiano mkubwa na kundi la kigaidi la Daesh tangu miaka mitatu iliopita.

Libya ilitumbukia katika vita vya ndani mwaka 2011 baada ya kuondolewa madarakani kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Muammar Gaddafi.