Ivory Coast na changamoto ya usalama kabla ya michezo ya Francophone
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i31998-ivory_coast_na_changamoto_ya_usalama_kabla_ya_michezo_ya_francophone
Maeneo mbalimbali ya Ivory Coast yameendelea kusumbuliwa na machafuko na hali ya ukosefu wa amani siku moja tu kabla ya kuanza mashindano ya michezo ya nchi wanachama katika jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa, Francophone.
(last modified 2025-11-07T02:31:33+00:00 )
Jul 20, 2017 03:41 UTC
  • Ivory Coast na changamoto ya usalama kabla ya michezo ya Francophone

Maeneo mbalimbali ya Ivory Coast yameendelea kusumbuliwa na machafuko na hali ya ukosefu wa amani siku moja tu kabla ya kuanza mashindano ya michezo ya nchi wanachama katika jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa, Francophone.

Ripoti zinasema kuwa, mashindano ya 8 ya michezo ya nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa yataanza kesho Ijumaa katika mji wa Abidjan huku baadhi ya maeneo ya nchi hiyo yakiendelea kuzongwa na machafuko na ukosefu wa amani.

Taarifa iliyotolewa na komandi ya jeshi la Ivory Coast imesema kuwa, watu watatu wameuawa na wengine 6 kujeruhiwa katika mapigano ya kufyatuliana risasi yaliyotokea karibu na kambi ya jeshi ya mji wa Korhogo. 

Ivory Coast

Kutokana na hali hiyo serikali ya Ivory Coast imetayarisha kikosi kinachojumuisha askari polisi, jeshi na skari usalama elfu 9 kwa ajili ya kulinda usalama mji Abidjan kunakofanyika mashindano hayo ya michezo ya Francophone. 

Awali waasi wa zamani ambao hadi sasa bado hawajajumuishwa katika jeshi la taifa la Ivory Coast walitishia katika mji wa Bouake kwamba, watavuruga mashindano hayo ya michezo iwapo hawatalipwa marupurupu yao.