Mabadiliko ya ghafla ya mawaziri nchini Kodivaa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i32012-mabadiliko_ya_ghafla_ya_mawaziri_nchini_kodivaa
Rais Alassane Ouattara wa ivory coast amefanya mabadiliko ya ghafla katika baraza lake la mawaziri.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 20, 2017 07:47 UTC
  • Rais Alassane Ouattara wa Kodivaa
    Rais Alassane Ouattara wa Kodivaa

Rais Alassane Ouattara wa ivory coast amefanya mabadiliko ya ghafla katika baraza lake la mawaziri.

Televisheni ya France 24 imeripoti habari hiyo na kusema kuwa, katika mabadiliko hayo, Ouattara amebadilisha mawaziri wa wizara mbili muhimu za Bajeti na Ulinzi.

Wanasiasa nchini Kodivaa wanasema kuwa, lengo la Rais Alassane Ouattara la kufanya mabadiliko hayo ni kuwatia nguvu watu wake wa karibu na kuleta mlingano wa fikra katika taasisi za utendaji. Ushahidi wa hayo ni jinsi Ouattara alivyomteua Amadou Coulibaly, Waziri Mkuu wa nchi hiyo kuchukua nafasi ya waziri wa bajeti sambamba kuendelea kuwa waziri mkuu.

Kwa mujibu wa habari hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani naye amebakishwa katika nafasi yake na kuongezewa wizara nyingine muhimu kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi wa Kodivaa.

Katika miezi ya hivi karibuni, nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika imekumbwa na misukosuko, machafuko na hata uasi wa wanajeshi.