Radiamali ya viongozi wa Ulaya kuhusu mgogoro wa wakimbizi wa Kiafrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i35503-radiamali_ya_viongozi_wa_ulaya_kuhusu_mgogoro_wa_wakimbizi_wa_kiafrika
Rais Emannuel Macron wa Ufaransa Jumamosi iliyopita aliarifu kuhusu kuasisiwa ofisi ya kuwapokea wakimbizi katika nchi mbili za Kiafrika. Alisema kuwa katika wiki zijazo kabla ya kumalizika mwezi huu wa Oktoba, ofisi hizo zitaasisiwa huko Chad na Niger kwa ajili ya kuwatambaua raia waliotimiza masharti ya kuwa wakimbizi.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Oct 11, 2017 08:13 UTC
  • Radiamali ya viongozi wa Ulaya kuhusu mgogoro wa wakimbizi wa Kiafrika

Rais Emannuel Macron wa Ufaransa Jumamosi iliyopita aliarifu kuhusu kuasisiwa ofisi ya kuwapokea wakimbizi katika nchi mbili za Kiafrika. Alisema kuwa katika wiki zijazo kabla ya kumalizika mwezi huu wa Oktoba, ofisi hizo zitaasisiwa huko Chad na Niger kwa ajili ya kuwatambaua raia waliotimiza masharti ya kuwa wakimbizi.

Akizungumza na Filippo Grandi Mkuu wa Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa huko Paris, Rais Macron amesisitiza kuwa raia walioomba hifadhi huko Chad na Niger watachaguliwa kutoka kwenye orodha iliyotayarishwa na umoja huo. 

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa (kulia) katika mazungumzo mjini Paris na Filippo Grandi  Mkuu wa Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya UN

Mgogoro wa wakimbizi na kundelea hali hiyo kuhususan kushtadi wimbi la wahamiaji haramu wanaotoka katika nchi za eneo la Sahel na kaskazini mwa Afrika kuelekea katika bahari ya Mediterrania na kuanzia hapo magenge ya magendo ya binadamu kuwavusha wahajiri hao haramu kwa kutumia boti na mitumbwi ya plastiki kuelelea Ulaya, kumezisababishia changamoto kubwa nchi za mpakani za Ulaya khususan Italia. Hasa ikizingatiwa kwamba Ufaransa pia ambayo iko katika pwani ya kaskazini mwa Mediterrania imegeuzwa na kuwa moja ya maeneo yanayokusudiwa na wahamiaji haramu. Kwa kuzingatia mafanikio ya kiwango fulani yaliyopatikana  katika kuwazuia wakimbizi  kupitia njia ya Uturuki kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Umoja wa Ulaya na Uturuki mwezi Machi mwaka 2016, umoja huo tayari umetafuta njia ya ufumbuzi sawa na hiyo kwa ajili ya kusitisha wimbi la wakimbizi wanaoelekea Ulaya kwa kutumia njia ya  bahari ya Mediterrania kwa kufikia mapatano na nchi za Kiafrika khususan Libya na Tunisia; na kwa njia hiyo nchi hizo zizuie wimbi la wakimbizi wanaoelekea katika nchi za kusini mwa Ulaya na khususan huko Italia. Hasa ikitiliwa maanani kuwa nchi kama Misri, Sudan na hivi sasa Chad na Niger pia zinapewa kipaumbele kama nchi zilizokusudiwa kutekeleza mipango inayohusiana na kuzuia wimbi la wahamiaji haramu. 

Katika uwanja huo, Nico Fried mwandishi habari wa Kijerumani ameashiria kulegeza msimamo kwa kiwango fulani Kansela wa Ujerumani Angela Merkel  kuhusu siasa zake za huko nyuma kuhusiana na suala wa wakimbizi na kueleza kuwa: Merkel ndiye anayeongoza mpango huo wa kuwazuia wakimbizi na amesaini makubaliano na Uturuki katika uwanja huo; na kupendekeza kuasisiwa vituo vya kuwahifadhi  wakimbizi ambao watafukuzwa huko Ulaya kufuatia safari aliyofanya katika nchi za Kiafrika na kuzikabidhi nchi hizo misaada ya kifedha. 

Angela Merkel, Kansela wa Ujerumani  

Hata hivyo nchi za Ulaya kama Ufaransa sasa zimefanikiwa kuwazuia wahajiri haramu katika nchi za asili kwa kuzingatia wimbi kubwa la wahamiaji hao kutoka katika nchi za eneo la Sahel barani Afrika; ambapo sasa tunashuhudia hatua iliyotekelezwa na serikali ya Ufaransa ya kuanzisha ofisi za kuwapokea wakimbizi huko Chad na Niger. Hivi sasa inaonekana kuwa licha ya siasa na hatua zilizochukuliwa na Umoja wa Ulaya, nchi muhimu za umoja huo kama Ujerumani, Ufaransa na Italia nazo zinafuatilia jitihada hizi kwa upekee ambapo kunashuhudiwa kufunguliwa ofisi hizo za kuwapokea wakimbizi huko Chad na Niger. Pamoja na hayo yote, kufanikiwa jitihada  hizo kutakuwa mashakani kikamilifu iwapo kutaendelea kuwepo wimbi la wahamiaji haramu kutoka katika nchi za Kiafrika kuelekea Ulaya.