Mayahudi waandamana London kupinga safari ya Netanyahu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i36115-mayahudi_waandamana_london_kupinga_safari_ya_netanyahu
Mayahudi wanaopinga utawala wa Kizayuni wa Israel wamefanya maandamano mjini Landon wakipinga safari ya Waziri Mkuu wa utawala huo nchini Uingereza.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 02, 2017 13:51 UTC
  • Mayahudi waandamana London kupinga safari ya Netanyahu

Mayahudi wanaopinga utawala wa Kizayuni wa Israel wamefanya maandamano mjini Landon wakipinga safari ya Waziri Mkuu wa utawala huo nchini Uingereza.

Makumi ya Mayahudi wanaopinga Uzayuni wameandamana mbele ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May mjini London wakipinga safari inayofanywa na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanhayu nchini humo. 

Waandamanaji wao wamefika mjini London wakitokea miji mbalimbali ya Uingereza kama Manchester, Stamford na kwengineko. 

Waziri Mkuu wa utawala katili wa Israel, Benjamin Netanyahu aliwasili London, Uingereza jana.

Watetezi wa haki za binadamu wapinga safari ya Netanyahu London

Tangu Netanyahu alipowasili mjini London, wanaharakati wa kutetea haki za binadamu na watetezi wa haki za taifa la Palestina wamekuwa wakifanya maandamano na harakati mbalimbali za kupinga safari hiyo na vilevile mazungumzo yake na maafisa wa serikali ya Uingereza.

Awali wanaharakati wa masuala ya kijamii na watetezi wa haki za watu wa Palestina waliitaka serikali ya London kufuta safari ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Isarel nchini Uingereza kutokana na jinai na mauaji yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya raia wa Palestina.