Chama tawala nchini Zimbabwe kuongoza maandamano dhidi ya Mugabe
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i36471-chama_tawala_nchini_zimbabwe_kuongoza_maandamano_dhidi_ya_mugabe
Chama tawala nchini Zimbabwe Zanu-PF hii leo klnatazamiwa kuongoza maandamano katika mji mkuu Harare, kumshinikiza Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo ajiuzulu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 17, 2017 23:50 UTC
  • Chama tawala nchini Zimbabwe kuongoza maandamano dhidi ya Mugabe

Chama tawala nchini Zimbabwe Zanu-PF hii leo klnatazamiwa kuongoza maandamano katika mji mkuu Harare, kumshinikiza Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo ajiuzulu.

Afisa mwandamizi wa chama hicho ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa, maandamano ya leo ni sehemu ya mikakati ya kumtaka Mugabe aachie ngazi haraka iwezekanavyo, baada ya kuitawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 37.

Wakati huo huo jeshi la Zimbabwe linamtaka Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo aondoke madarakani kwa amani na kuruhusu serikali ya mpito chini ya uongozi wa aliyekuwa makamu wake, Emmerson Mnangagwa, ambaye alimtimua kazi wiki iliyopita.

Maandamano wa wapinzani dhidi ya Mugabe miezi michache iliyopita

Lengo la hatua hiyo ya jeshi ambalo linashikilia madaraka kwa sasa ni kuzuia jario la aina yoyote la Robert Mugabe la kumkabidhi madaraka mkewe, Grace Mugabe.

Wakati huo huo, Chris Mutsvangwa, kiongozi wa maveterani wa nchi hiyo kamwe Mugabe hatoruhusiwa kupinga msimamo wa jeshi la nchi hiyo na kuendelea kung'ang'ania madaraka.