Wabunge wa Tunisia wakosoa taarifa ya Arab League dhidi ya Iran, Hizbullah
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i36753-wabunge_wa_tunisia_wakosoa_taarifa_ya_arab_league_dhidi_ya_iran_hizbullah
Kundi la Wabunge wa Tunisia limekosoa taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu chini mashinikizo ya Saudi Arabia dhidi ya harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon Hizbullah na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 24, 2017 13:05 UTC
  • Wabunge wa Tunisia wakosoa taarifa ya Arab League dhidi ya Iran, Hizbullah

Kundi la Wabunge wa Tunisia limekosoa taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu chini mashinikizo ya Saudi Arabia dhidi ya harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon Hizbullah na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Nchi wanachama wa Arab League zilikutana mjini Cairo nchini Misri Jumapili iliyopita, kufuatia ombi la Saudia la kutaka eti 'kupigishwa magoti Iran na Hizbullah'.

Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu mwishoni mwa mkutano huo ilidai kuwa, Tehran inaingilia masuala ya ndani ya nchi za Kiarabu na kuvuruga usalama na uthabiti katika eneo. Aidha taarifa hiyo ya Arab League iliiorodhesha harakati ya Kiislamu ya Hizbullah kama shirika la kigaidi.

Wabunge zaidi ya 40 wa Tunisia wamesaini hati ya kulaani taarifa hiyo ya kichochezi ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, huku wakimtaka Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika kufuta uungaji mkono wa nchi hiyo kwa taarifa hiyo.

Bunge la Tunisia

Hivi karibuni, Youssef Chahed, Waziri Mkuu wa Tunisia alikosoa hatua ya kuibua migogoro ya Saudia katika nchi nyingine hususan Lebanon na kusema kuwa anataraji kwamba mzozo huo hautapelekea kutokea vita kati ya nchi mbili hizo.

Aliyasema hayo baada ya Saad Hariri, Waziri Mkuu wa Lebanon kutangaza kujiuzulu akiwa nchini Saudi Arabia sambamba na Riyadh kuwataka raia wake kuondoka Lebanon mara moja.

Wadadisi wa mambo wanasema Saudia inajaribu kuituhumu harakati ya Hizbullah na kuibua mzozo kati ya viongozi wa kisiasa wa Lebanon kwa shabaha ya kupanua satwa yake ndani ya nchi hiyo.