AU yafanya kikao cha kuzungumzia hali ya wakimbizi nchini Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i37177-au_yafanya_kikao_cha_kuzungumzia_hali_ya_wakimbizi_nchini_libya
Umoja wa Afrika AU umeitisha kikao cha kuchunguza hatua za kivitendo za kuwakomboa wahamiaji wa Kiafrika katika jela za Libya na kuwarejesha katika nchi zao.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Dec 04, 2017 11:40 UTC
  • AU yafanya kikao cha kuzungumzia hali ya wakimbizi nchini Libya

Umoja wa Afrika AU umeitisha kikao cha kuchunguza hatua za kivitendo za kuwakomboa wahamiaji wa Kiafrika katika jela za Libya na kuwarejesha katika nchi zao.

Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCER na shirika la kimataifa la wahajiri, yameonana leo Jumatatu tarehe 4 Disemba na kuzungumzia njia za ukombozi wa wahajiri wa Afrika katika jela za Libya. 

Katika kikao hicho, kumejadiliwa namna ya kuandaa mazingira mazuri ya kurejeshwa katika nchi zao wahajiri wa Afrika kutoka katika jela za Libya.

Wahamiaji haramu nchini Libya

 

Lengo jingine la kikao hicho cha Addis Ababa ni kuunda muungano utakaoongozwa na Umoja wa Afrika kwa ajili ya kupambana na maafa ya kibinadamu nchini Libya.

Kutumwa kikosi cha operesheni ndani ya Libya na kuwakomboa wahajiri 15 elfu wa Kiafrika kutoka katika jela za nchi hiyo hadi mwishoni mwa mwezi huu wa Disemba, ni miongoni mwa kazi kuu zitakazofanywa na muungano huo.

Video zilizoenea ulimwenguni zikionesha wahajiri wa Kiafrika wakipigwa mnada na kuuzwa kama bidhaa katika masoko ya Libya zimeamsha hasira kubwa za jamii ya kimataifa.

Katika kupinga vikali jinai hiyo dhidi ya binadamu, Umoja wa Afrika umetoa mwito wa kuachiliwa haraka wahajiri hao kutoka katika jela za Libya na kurejeshwa makwao kwa ushirikiano wa washiriki wa kikao cha mjini Addis Ababa, Ethiopia.