Tahadhari yatolewa kuhusu kuenea ugonjwa wa malaria barani Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i39531-tahadhari_yatolewa_kuhusu_kuenea_ugonjwa_wa_malaria_barani_afrika
Viongozi wa Umoja wa Afrika na wa Shirika la Afya Duniani WHO wametahadharisha kuhusiana na uwezekano wa kuenea na kusambaa zaidi ugonjwa wa malaria barani Afrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 27, 2018 01:04 UTC
  • Tahadhari yatolewa kuhusu kuenea ugonjwa wa malaria barani Afrika

Viongozi wa Umoja wa Afrika na wa Shirika la Afya Duniani WHO wametahadharisha kuhusiana na uwezekano wa kuenea na kusambaa zaidi ugonjwa wa malaria barani Afrika.

Tahadhari hiyo imetolewa na viongozi wa Umoja wa Afrika na wa Shirika la Afya Duniani WHO katika mkutano wao uliofanyika jana huko Addis Ababa Ethiopia yalipo makao makuu wa Umoja wa Afrika AU.

Viongozi hao wametangaza kuwa, ugonjwa wa malaria ungali changamoto kubwa kkabisa barani Afrika.

Moussa Faki Mahamat, Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika amesema katika kikao hicho kwamba, kuna haja ya kuchukuliwa hatua za pande zote kwa shabaha ya kukabiliana na ugonjwa huo hususan barani Afrika.

Chanjo ya Malaria

Afisa huyo wa ngazi za juu wa Umoja wa Afrika amesema kuwa, ugonjwa wa malaria umekuwa na taathira hasi katika uwanja wa masuala ya afya, uchumi na jamii na hata katika kuenea umasikini.

Malaria ni ugonjwa wa kuambukiza ambao unaambukizwa na mbu wa jenasi Anopheles na kusababishwa na kidubini aina ya protisti Plasmodium. Mara nyingi ugonjwa huo huitwa "homa" tu, ingawa homa ni dalili yake mojawapo tu, pia kuna magonjwa mengi yanayosababisha homa. Malaria yanaokea katika maeneo ya kitropiki na yanayokaribia tropiki ikiwa ni pamoja na sehemu za AmerikaAsia na Afrika.