Wakimbizi 36 kutoka DRC wafariki Uganda kutokana na ugonjwa wa kipindupindu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i42030-wakimbizi_36_kutoka_drc_wafariki_uganda_kutokana_na_ugonjwa_wa_kipindupindu
Wakimbizi 36 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamefariki kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu uliotokea magharibi mwa Uganda mwezi uliopita.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 22, 2018 11:31 UTC
  • Wakimbizi 36 kutoka DRC wafariki Uganda kutokana na ugonjwa wa kipindupindu

Wakimbizi 36 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamefariki kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu uliotokea magharibi mwa Uganda mwezi uliopita.

Taarifa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) imesema, jumla ya kesi za ugonjwa huo zilizoripotiwa ni 1,747, kati yao 36 wamefariki tangu Februari 23 mwaka huu, wakati mlipuko wa ugonjwa huo ulipotokea kwenye kambi ya wakimbizi katika wilaya za kusini magharibi za Hoima na Kyegegwa.

Jumatatu wiki hii, wagonjwa wapya wa kipindupindu walipokewa katika kituo cha kutibu ugonjwa huo, wengi wao wakiwa wakimbizi wapya ambao wamekimbia mapigano kati ya makabila ya Lendu na Hema nchini DRC.

Wakimbizi waliouguwa kipindupindu

Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa, imesema kuwa mapigano hayo ya kikabila hadi sasa yamesababisha kwa akali watu 150 kuuawa na wengine elfu 32 kuyahama makazi yao na kwenda maeneo mengine ya nchi hiyo, huku watu elfu 28 wengine wakiwa wakimbizi katika nchi jirani hususan Uganda. Kwa miaka kadhaa makundi ya kikabila ya Lindu na Hema yamekuwa na mizozo ya silaha ambapo maelfu ya watu wameuawa kufuatia mapigano kati yao yaliyoanza tangu mwaka 1999.