Wazayuni wazuia kusomwa adhana katika Haram ya Nabii Ibrahim AS
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i4333-wazayuni_wazuia_kusomwa_adhana_katika_haram_ya_nabii_ibrahim_as
Wizara ya Wakfu ya Palestina imetangaza kuwa, mwezi uliopita wa Machi, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni walizuia mara chungu nzima kusomwa adhana katika Haram ya Nabii Ibrahim AS mjini Alkhalil.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 03, 2016 07:31 UTC
  • Wazayuni wazuia kusomwa adhana katika Haram ya Nabii Ibrahim AS

Wizara ya Wakfu ya Palestina imetangaza kuwa, mwezi uliopita wa Machi, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni walizuia mara chungu nzima kusomwa adhana katika Haram ya Nabii Ibrahim AS mjini Alkhalil.

Shirika la habari la Palestina MA'A limemnukuu Waziri wa Waqfu wa Palestina akisema kuwa, utawala wa Kizayuni unafanya njama za kuuyahudisha msikiti wa Ibrahimi katika mji wa Alkhalil na kuongeza kuwa, katika mwezi uliopita, utawala huo ghasibu ulizuia mara 51 kusomwa adhana msikitini humo.

Waziri wa Waqfu wa Palestina amesema kuwa, kitendo cha Wazayuni cha kuzuia kusomwa adhana katika msikiti huo ni muendelezo wa jinai za Wazayuni hao za kuvunjia heshima matukufu ya Waislamu na kuongeza kuwa, wanajeshi wa Israel waliweka kizuizi katika lango kuu la kuingilia msikitini humo ili kuwazuia Waislamu wasiingie msikitini humo.

Mara nyingi utawala wa Kizayuni unadai kuwa eti sauti ya adhana inawakera Mayahudi na ndio maana unapiga marufuku kusomwa adhana misikitini.

Si hayo tu, lakini pia wanajeshi wa utawala wa Kizayuni mara nyingi huwa wanaufunga msikiti wa Nabii Ibrahimi AS huko Alkhalil katika muda wote wa mapumziko ya sikukuu za Mayahudi. Utawala wa Kizayuni umepasisha sheria ya kuzuia kusomwa adhana katika maeneo matakatifu ya Waislamu wa Palestina.