Boko Haram 300 wauawa, raia 2000 wakombolewa
Muungano wa kijeshi unaopambana na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Boko Haram umetangaza kuwa, wapiganaji 300 wa kundi hilo wameangamizwa na karibu raia 2000 wasio na hatia wamekombolewa kutoka mikononi mwa magaidi hao.
Muungano huo umetangaza kuwa wapiganaji hao 300 wa kundi la kigaidi la Boko Haram wameuawa katika operesheni ya kijeshi iliyofanyika karibu na mpaka wa Nigeria na nchi za Cameroon na Chad.
Kamanda Mcanerooni wa operesheni hiyo, Bouba Dobekreo, amesema kuwa operesheni hiyo imelenga na kuharibu kabisa kambi ya Boko Haram iliyokuwa ikitumiwa kutengeza mabomu iliyopo yapata kilomita 35 kutoka kwenye mji wa Kumshe na kwamba magari na zana za kijeshi za kundi hilo zimechukuliwa ngawira.
Askari 9000 wanashiriki katika muungano dhidi ya Boko Haram unaoshirikisha nchi za Cameroon, Nigeria, Chad, Niger na Benin.