18 wafariki dunia katika mafuriko Ivory Coast
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i46104-18_wafariki_dunia_katika_mafuriko_ivory_coast
Watu 18 wamefariki dunia katika mji mkuu wa Ivory Coast, Abidjan katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua kali.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 20, 2018 16:33 UTC
  • 18 wafariki dunia katika mafuriko Ivory Coast

Watu 18 wamefariki dunia katika mji mkuu wa Ivory Coast, Abidjan katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua kali.

Ripoti zinasema kuwa mafuriko hayo pia yamesababisha maafa na hasara za mali ya umma.

Wakazi wa Abidjan wamewataka maafisa wa serikali ya Ivory Coast kushughulikia watu waliopatwa na maafa wakisisitiza kuwa tatizo hilo limekuwepo kwa miaka mingi bila ya kuchukuliwa hatua zozote za maana za kukabiliana nalo.

Utabiri wa hali ya hewa unaonesha kuwa mvua kali zitaendele akunyesha nchini Ivory Coast na kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kutokea tena mafuriko katika mji mkuu wa nchi hiyo na maeneo mengine. 

Maafisa wa serikali ya Ivory Coast wamewataka wakazi wa mji mkuu wa nchi hiyo kuchukua tahadhari.