Afrika Kusini nayo yajibu mashinikizo ya kiuchumi ya Marekani dhidi yake
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i47613-afrika_kusini_nayo_yajibu_mashinikizo_ya_kiuchumi_ya_marekani_dhidi_yake
Serikali ya Afrika Kusini imelalamikia vikali mashinikizo ya serikali ya Marekani dhidi ya uchumi wa nchi hiyo na imeamua kutopeleka tena mifugo yake ya jamii ya kuku huko Marekani kama njia ya kupinga ushuru mpya ziliowekewa bidhaa zake na serikali ya Donald Trump.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 22, 2018 09:57 UTC
  • Afrika Kusini nayo yajibu mashinikizo ya kiuchumi ya Marekani dhidi yake

Serikali ya Afrika Kusini imelalamikia vikali mashinikizo ya serikali ya Marekani dhidi ya uchumi wa nchi hiyo na imeamua kutopeleka tena mifugo yake ya jamii ya kuku huko Marekani kama njia ya kupinga ushuru mpya ziliowekewa bidhaa zake na serikali ya Donald Trump.

Jumuiya ya wafugaji wa mifugo ya jamii ya kuku nchini Afrika Kusini imepasisha hatua ya kisheria ya kupiga marufuku kupeleka nchini Marekani mifugo ya jamii ya kuku kutoka Afrika Kusini. 

Martínus Stader, mmoja wa viongozi wa jumuiya ya kufuga kuku na jamii ya mifugo hiyo huko Afrika Kusini amesema kuwa, hatua hiyo ni majibu kwa uamuzi wa Donald Trump wa kuzipandishia ushuru bidhaa za feleji na alumini zinazoingizwa Marekani kutokea Afrika Kusini.

Amesema, siasa mpya za ushuru za Marekani zinakanyaga makubaliano ya mwaka 2015 yaliyofikiwa baina ya nchi hiyo na Afrika Kusini.

Siasa za serikali ya Donald Trump za kuweka vikwazo, kuongeza ushuru na mashinikizo ya kiuchumi dhidi ya nchi nyingine ambazo zinatekelezwa kwa madai kuwa nchi hizo zinapinga siasa Marekani, zinaendelea kukumbwa na majibu mbalimbali makali katika kona zote za dunia.