Oct 07, 2018 07:46 UTC
  • Wananchi wa Cameroon wapiga kura, Rais Biya (85) awania muhula wa 7

Wananchi wa Cameroon waliotimiza masharti ya kupiga kura mapema leo wameelekea katika masanduku ya kupigia kura katika uchaguzi mkuu wa rais, huku kinara wa chama cha PURS, Serge Espoir Matomba akikanusha taarifa kuwa amejiunga na muungano wa upinzani unaochuana na Rais Paul Biya.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mwendo wa saa mbili asubuhi kwa saa za nchi hiyo na vinatazamiwa kufungwa saa kumi na mbili jioni.

Tume ya Uchaguzi nchini humo ELECAM imepinga ombi la kujiondoa katika kinyang'anyiro hicho mgombeaji wa chama cha People's Development Front (FDP), Akere Muna, akisema kuwa hoja yake haina msingi wa kisheria.

Wananchi milioni sita wa Cameroon wametimiza masharti ya kushiriki zoezi hilo la kidemokrasia.

 

Rais Paul Biya

Muna hapo jana alitangaza kujiondoa na kusema kuwa atamuunga mkono mgombea mwenzake Maurice Kamto wa chama cha Movement for the Rebirth of Cameroon MRC.

Rais Paul Biya mwenye umri wa miaka 85 na ambaye yuko madarakani kwa karibu miaka 36 sasa anagombea muhula wa saba wa miaka saba. 

Tags