Jun 16, 2024 06:11 UTC
  • Rwanda yachapisha orodha ya mwisho ya wagombea 3 wa urais na zaidi ya wagombea 500 wa ubunge

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Rwanda imetangtaza orodha ya mwisho ya wagombeaji wa uchaguzi wa rais na wabunge uliopangwa kufanyika mwezi ujao.

Wagombea watatu wa urais waliotangazwa kwenye orodha ya muda ni pamoja na Rais wa hivi sasa Paul Kagame wa chama tawala cha RPF, Frank Habineza wa chama cha upinzani cha Democratic Green Party of Rwanda na Philippe Mpayimana, mgombea binafsi.

Tume hiyo pia iliwaidhinisha pia zaidi ya wagombea 500 kuchuana kwa ajili ya viti 80 vya Bunge.

Muungano wa RPF na vyama vingine vina wagombea wengi zaidi wa ubunge.

Wagombea tisa wa urais na karibu 700 wa ubunge waliwasilisha maombi yao ya kugombea lakini wamechujwa na kubakishwa wabombea watatu wa urais na 500 wa ubunge.

Uchaguzi Mkuu wa Rais na Bunge nchini Rwanda umepangwa kufanyika tarehe 15 mwezi ujao wa Julai. 

Takriban Wanyarwanda milioni 9.5 wametimiza masharti ya kupiga kura katika uchaguzi wa rais na wabunge.

Tags