Oct 09, 2018 02:43 UTC
  • Mgombea wa upinzani ajitangaza mshindi wa uchaguzi wa rais Cameroon

Mgombea wa urais wa chama cha upinzani cha Movement for the Rebirth of Cameroon (MRC), Maurice Kamto amejitangaza mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika Jumapili tarehe 7 Oktoba.

Katika kikao na waandishi wa habari katika mji mkuu Yaounde hapo jana, Kamto amesema, "Lengo langu lilikuwa kupiga penati. Nimefanya hivyo na nikufunga bao. Hivyo basi namuomba rais anayeondoka kuandaa mchakato wa amani wa kukabidhi madaraka."

Hata hivyo Paul Atanga, Waziri wa Utawala wa Ndani nchini humo amesema Baraza la Katiba ndicho chombo pekee cha sheria chenye mamlaka ya kumtangaza mshindi wa uchaguzi huo.

Rais Paul Biya mwenye umri wa miaka 85

 

Baadhi ya vyama vya upinzani viliungana siku moja kabla ya uchaguzi huo ili kupambana na Rais Paul Biya mwenye umri wa miaka 85 na ambaye yuko madarakani kwa karibu miaka 36 sasa. 

Hii ni katika hali ambayo, watu wasiopungua watano wameuawa katika machafuko yaliyotokea wakati wa kupiga kura katika eneo la Bafut lenye wazungumzaji wengi wa lugha ya Kiingereza ambalo linapigania kujitenga nchini Cameroon

Tags