Russia kufungua kituo cha kijeshi Jamhuri ya Afrika ya Kati
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i50794-russia_kufungua_kituo_cha_kijeshi_jamhuri_ya_afrika_ya_kati
Russia inatafakari kufungua kituo cha kijeshi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambako tayari Moscow inaendelea kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa nchi hiyo ya Kiafrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 11, 2019 12:25 UTC
  • Russia kufungua kituo cha kijeshi Jamhuri ya Afrika ya Kati

Russia inatafakari kufungua kituo cha kijeshi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambako tayari Moscow inaendelea kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa nchi hiyo ya Kiafrika.

Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Marie-Noelle Koyara ameliambia shirika la habari la Russia la RIA Novosti kwamba, kuanzishwa kambi ya kijeshi ya Russia katika nchi hiyo ni jambo linalowezekana, chini ya makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi yaliyosainiwa hivi karibuni katika ya nchi mbili hizo.

Amesema "Wananchi wetu wana mtazamo chanya na mzuri kwa Russia. Wakati ambapo mazungumzo ni kuhusu Russia, wananchi wa taifa hili huwa waelewa na kuwa na matumaini kuwa uhusiano na ushirikiano wa Moscow na Bangui utabadilisha mustakabali wa nchi hiyo.

Uhusiano wa kijeshi unaokuwa wa Russia na Jamhuri ya Afrika ya Kati na hamu kubwa ya Moscow ya kujikita barani Afrika viliakisiwa pakubwa mwezi Julai mwaka uliomalizika, wakati waandishi habari wawili wa Russia walipouliwa wakati wakichunguza madai ya kuwepo mamluki wa Russia nchini humo.

Waziri wa Ulinzi wa CAR, Marie-Noelle Koyara

Makubaliano hayo yalisainiwa katika maonyesho ya silaha ya taifa karibu na Moscow na kuhudhuriwa na Mawaziri wa Ulinzi wa nchi mbili hizo.

Mwaka uliopita Russia ilituma silaha nyepesi kwa vikosi vya usalama vya Jamhuri ya Afrika ya Kati sanjari na kutuma nchini humo walimu wa kijeshi na kiraia 175 kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vikosi hivyo.