Shambulio la anga la Marekani laua watu 6 nchini Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i59694-shambulio_la_anga_la_marekani_laua_watu_6_nchini_somalia
Watu sita wasio na hatia wameuawa nchini Somalia baada ya basi lao kushambuliwa na ndege zisizo na rubani (drone) za Marekani katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika iliyoathiriwa vibaya na vita.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 12, 2020 04:28 UTC
  • Shambulio la anga la Marekani laua watu 6 nchini Somalia

Watu sita wasio na hatia wameuawa nchini Somalia baada ya basi lao kushambuliwa na ndege zisizo na rubani (drone) za Marekani katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika iliyoathiriwa vibaya na vita.

Mbunge mmoja wa Somalia ametangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, jana Jumatano droni za Marekani zilishambulia basi moja na kuua raia sita akiwemo mtoto mdogo mmoja na wala si magaidi wa al Shabab kama inavyodai Marekani.

Mmoja wa raia hao wa Somalia aliyeuawa katika shambulio hilo la kijinai la Marekani ni mtoto wa miaka 13.

Marekani ina historia mbovu ya kuua watu wasio na hatia katika nchi mbalimbali duniani kwa madai ya kupambana na ugaidi na mara zote wananchi na tawala za nchi hizo zinalaani na kulalamikia jinai hizo za Marekani.

Ndege isiyo na rubani ya Marekani. Nchi hiyo inashutumiwa sana kwa kufanya mauaji ya kiholela katika pembe mbalimbali za dunia kwa kutumia ndege za aina hii

 

Tangu mwaka 2007, kundi la kigaidi la al Shabab lenye mfungamano na mtandao wa al Qaida limekuwa likifanya mashambulizi ndani ya Somalia kwa lengo la kuiangusha serikali kuu ya nchi hiyo inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Ijapokuwa mwaka 2011 genge hilo lilifurushwa kutoka kwenye miji mikubwa ya Somalia, lakini bado linadhibiti maeneo ya ndani ya vijijini ambako ni vigumu kufikiwa na wanajeshi wa serikali na wale wa kimataifa.

Marekani inadai kuendesha mashambulizi dhidi ya al Shabab kama njia ya eti kuisaidia serikali kuu ya Somalia.