Jeshi la Somalia laua magaidi wengine 7 wa al-Shabaab
(last modified Wed, 27 May 2020 03:39:18 GMT )
May 27, 2020 03:39 UTC
  • Jeshi la Somalia laua magaidi wengine 7 wa al-Shabaab

Jeshi la Taifa la Somalia limefanikiwa kuangamiza wanachama saba wa kundi la kigaidi la al-Shabaab katika eneo la Hiran, katikati mwa nchi.

Mohamud Hassan Ibrahim, kamanda mkuu wa kikosi cha 22 cha jeshi la Somalia amesema magaidi hao wa al-Shabaab waliuawa jana Jumanne katika operesheni iliyolenga maficho ya genge hilo la ukufurishaji katika eneo la Hiran.

Kadhalika wanachama wengine kadhaa wa kundi hilo wamejeruhiwa katika operesheni hiyo ya jana Jumanne.

Operesheni hiyo imejiri siku moja baada ya jeshi la eneo lenye mamlaka ya ndani la Jubaland kutangaza habari ya kuangamiza wanachama wanne wa kundi hilo la kigaidi katika mji wa Dhobley, Kusini mwa Somalia.

Wanachama wa genge la kigaidi la al-Shabaab

Kundi hilo la kigaidi lilihusika na shambulizi la bomu katika mji wa Baidoa, kusini mwa nchi hiyo usiku wa kuamkia Jumatatu iliyopita wakati wa sherehe za Idul-Fitr, ambapo watu watano waliuawa na wengine 20 kujeruhiwa.

Kundi la al-Shabaab lenye mfungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaidah limehusika na utegaji mabomu na mashambulizi mengi ndani ya Somalia na katika nchi jiran tokea mwaka 2007.

 

Tags