Kamanda wa al Shabab aangamizwa katika operesheni ya jeshi la Somalia
(last modified Fri, 26 Jun 2020 06:43:04 GMT )
Jun 26, 2020 06:43 UTC
  • Kamanda wa al Shabab aangamizwa katika operesheni ya jeshi la Somalia

Redio ya serikali ya Somalia imetangaza kuwa jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kumuangamiza kamanda wa wanamgambo wa kundi la al Shabab.

Taarifa hiyo imesema Ashraf Azmi Abu Hamdan ameuawa katika operesheni ya kijeshi iliyopfanyika katika mkoa wa Juba ya Kati huko kusini mwa Somalia. Wapiganaji wengine watatu wa kundi hilo pia wameangamizwa katika operesheni hiyo.

Ashraf Azmi Abu Hamdan, ambaye ni kutoka Nepal, alikuwa mkufunzi mwandamizi katika kikundi hicho cha al Shabab.

Kundi hilo limekuwa likipigania kuipindua serikali kuu ya Somalia tangu 2008 na kuanzisha utawala wa "khilafa" kulingana na tafsiri yake isiyo sahihi ya sheria na mafundisho ya Uislamu.

Siku chache zilizopita pia wanachama wasiopungua 27 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabab waliuawa katika operesheni kadhaa zilizofanywa na jeshi la Somalia katika eneo la Shebelle Kusini mwa nchi.

Tags